Thursday, December 20, 2012

Afunga Ngono na Wanawake Wanne kwa mpigo

Wakati Bwana Laizer kama ilivyoshuhudiwa hapo chini alijitwalia Nancy wake (m'1 pekee) kwa maisha,Jumamosi iliyopita mwanaume mmoja wa nchini Afrika Kusini anayekwenda kwa jina la Milton Mbhele alijipatia umaarufu wa ghafla Duniani baada ya kufunga ndoa na wanawake wanne kwa mpigo.


Bwana Mbhele aliyewasili Harusini hapo akiwa kwenye gari nyeupe aina ya Limousine na Ma'Bibi zake, aliwavalisha pete za ndoa na kuwapiga mabusu ya nguvu Ma'bibi Harusi wake hao katika harusi kubwa na ya kukata na shoka iliyohudhuriwa na mamia ya watu.


Nchini Afrika kusini sheria zinaruhusu ndoa za wake wengiwengi na ndo maana hata Rais wa Afrika Kusini Jackob Zuma ana wake watatu.Utamaduni huu ni wa kawaida kwa makabila ya Zulu na Swazi.

No comments:

Post a Comment