Thursday, June 28, 2012

Mapenzi-jinsi ya kupata demu


Ili mdada akupende inategemea vitu vingi sana ambavyo vinasababisha wakupende.

1. jiografia: sehemu wadada walipo. wanachopenda wadada wa tanzania ni tofauti na wanachopenda wadada wamerekani na nitofauti na wanachopenda wadada wakichina

2. kipindi: kipindi wadada walichopo nacho kinategemewa sana, wadada wa enzi za mawe walikuwa wanapenda vitu vofauti na wadada wa enzi za miaka ya giza (dark ages), na

pia ni tofauti na wadada wa enzi zetu ja JF na FB na SIMU.

3. jenetiks: huyo mdada kazaliwa kwenye familia gani pia inatofautisha....kivipi?....wa dada wengi wanatafuta wanaume wanaofanana na baba zao. Kwa hiyo mwanaume ukiwa

na tabia zinazofanana na tabia za baba wa mdada fulani, basi huo mdada atakupenda.

Sasa kuna kupendwa kwa aina mbili:
1. kuonyeshwa mapenzi
2. kupendwa kwa dhati

Ingawa watu wengi sana wanasema wanataka mapenzi ya dhati, lakini ukweli ni kwamba watu wengi wanataka kuonyeshwa mapenzi tu.

Kuna tofauti kati ya kupendwa kwa dhati na kuonyeshwa mapenzi. Mdada anayekupenda kwa dhati, saa nyingine anaweza kufanya vitu ambavyo unaweza kudhani kuwa hakupendi.

Na hii inatokana na udhaifu wa binadamu kushindwa kuona kilichopo ndani ya moyo au akili ya mtu.

Kuonyeshwa mapenzi ni rahisi zaidi. Mfano mzuri ni kwenye movie. Nadhani ukiangalia zile romantic movies, baada ya dakika kadhaa utasema kuwa yule mdada anampenda yule

mkaka. Na unasema hivyo kwa sababu, unaona matendo yao...ingawa kikwelikweli wanaakti tu!

Kumbe basi unaweza kuigiza kuwa unampenda mtu, na huyo mtu na watu wengine wakadhani kuwa ni kweli kuwa unampenda.

Sasa kama unataka kuonyeshwa mapenzi (sio kupendwa kwa dhati), unachotakiwa kumfanyia mdada ni:
1. Mnunulie vitu...mnunulie kila kitu anachosema anataka, simu, umpe vocha, mpe nauli, na kadhalika.
2. Muonyeshe kuwa we unanguvu kuliko watu waliokuzunguka. Kiasi kwamba awe na wewe kwa ajili ya ulinzi.
3. vitu vingine nitatoa badae, mda umeisha.....nikirudi nitaelezea na vitu vya kufanya ili upendwe kwa dhati na sio kisanii.

Source

No comments:

Post a Comment