Friday, March 27, 2009

Shahawa na Mimba

Shahawa na Mimba

Baadhi ya watu wanadhani au wanaamini kuwa Shahawa huishi ndani ya mwili wa mwanamke kwa masaa 72 ambayo ni sawa na siku tatu, lakini ukweli ni kuwa Shahawa huzunguuka nakushambulia "Womb" ili zikakutane na yai ili kuwa kiumbe kwa muda wa siku saba.

Ndio maana wale wenzangu wanaotumia njia ya asilia ya kuzuia mimba
huwa wanashangaa nakuchanganyikiwa pale wanapogundua wamenasa wakati siku zilikuwa "salama", unatakiwa kufanya mahesabu yako vema....vinginevyo Tumia Condom

Vilevile kuna wale wanaotumia Condom baada ya mwanaume kuonja bila chuku-chuku alafu wanakuja shangaa au kataa mimba na kudai kuwa walifanya kwa kutumia kinga (Condom).....tambua kuwa yale maji-maji yenye uterezi na radha ya chumvi-chumvi yanayojitokeza kutokana na nyege pale kwenye jicho la uume hubeba shahawa pia.

Tambua kuwa tone la shahawa lenye ukubwa wa nukta hubeba karibu mbegu elfu moja na mia tano(1,500)......sasa niambie maji-maji yale yanabeba "nukta" ngapi za Shahawa?

No comments:

Post a Comment